SERUKALI Mkoani Njombe imewataka wakulima na
Wafanyabiashara kuitumia fursa ya kuuza zao la mahindi Nje ya Nchi baada ya kurahisishwa kwa upatikaniji wa
vibali ambavyo kwa sasa vinatolewa na makatibu wa tawala
wa Mikoa tofauti na awali vilikuwa vinatolewa na wizara
ya viwanda na biashara.
Akizungumza na East Africa Radio Afisa kilimo Mkoa wa
Njombe Awariywa Nnko amesema kuwa kila mfanyabiashara anaruhusiwa kuuza mazao
yake nje ya nchi kwa kufuata masharti yaliyoweka wakati wa ukataji wa kibali.
Hatua hii imekuja
kufuatia kuwepo kwa mrundikano wa mavuno ya mahindi yaliyokosa soko wakati hali
ya uzalishaji wa mahindi kwa mwaka 2013/14 jumla ya tani 411,802 zilizalishwa
katika mkoa wa Njombe.
Aidha Nnko amesema kuwa licha ya Wakala wa Hifadhi ya
Chakula ya Taifa NFRA tawi la
makambako kufanikiwa kununua tani 26,116
za mahindi hadi kufikia Novemba 5 mwaka huu sawa na asilimia 6.3 ya mavuno ya mahindi
hivyo kufunguliwa kwa soko hilo kutasaidia wananchi kuuza mazao yao na kusababisha
mahidi kupanda bei iliyo kuwa ikitarajiwa na wananchi.