WATOTO wawli wamedaiwa Kubakwa katika matukio mawili tofauti
mkoani Njombe likiwemo la Mtoto wa miaka 4 mkazi wa kijiji cha Imalinyi Mkoani
hapa kubakwa na mtoto wa miaka 15.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani,
akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa mtoto (4) mmoja (Jina
limehifadhiwa)mkazi wa kijiji cha Imalinyi wilaya ya Wang’ombe anadaiwa kubakwa
na mtoto mwenye umri wa miaka 15.
Alimtaja mtuhumiwa katika tukio la kwanza kuwa ni Boniface
Mbilinyi (15) mkazi wa kijiji cha Imalinyi wilaya ya Wanging’ombe Mkoani hapa
na kuwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 2:00 usiku.
Ngonyani alisema kuwa Mtoto huyo alibakwa akiwa nyumbani
kwao katika kijiji hicho hiyo na kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi hilo
wakati upelelezi wa tukio hilo unaendelea na kuwa atafikisha mahakamani
uchunguzi ukikamilika.
Kamanda alisema kuwa
katika tukio la pili jeshi la Polisi mkoa wa Njombe lilimkamata James Mhagama (43)
kwa tuhuma za kubaka mtoto wa miaka 14 (Jina limehifadhiwa) mkazi wa Milo
wilaya ya Njombe.
Alisema kuwa mtoto huyo ni mwanafunzi wa daraza la tano katika
shule moja wilayani Njombe (Jina limehifadhiwa ) na kuwa tukio hilo lilitokea
majira ya saa 12)) asubuhi.
Alisema kuwa mtoto huyo alibakwa akiwa karibu na nyumbani
kwao majira hayo ya asubuhi wakati akielekea shuleni.
Ngonyani alisema kuwa mtuhumiwa atapandishwa mahakamani
haraka baada ya upelezezi kukamilina ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.