SELINA Henry Bedebede ambaye ni mjasiliamali alizaliwa Juni
6, 1966 katika wilaya ya Morogoro vijijini eneo la Matombo.
Yeye ni mtoto wanne kati ya watoto saba wa Familia ya Mzee
Henry Bedebede na Bi Katelina Lawrence
wa kabila la Waruguru.
Alianza darasa la kwanza mwaka 1975 mpaka mwaka 1981 alipo
hitimu darasa la saba katika shule ya msingi Kilakala ya Mkoani Morogoro.
Anasema alianza kazi yake ya ujasiliamali tokea alipo kuwa
mtoto wa darasa la kwanza mwaka 1975.
Alisema kazi hiyo ya ujasiliamali alifundishwa na mamayake
mzazi aitwae Katelina, ambaye alikuwa akimtuma kwenda kuuza bidhaa katika
Chumba chao cha biashara kilichokuwa maeneo ya Kwa Mnyonge Kichangani, Morogoro
Mjini.
Bidhaa alizo kuwa akiziuza Selina ni pamoja na Togwa, Mafuta
ya Nazi, pamoja na Mboga za majani zilizo sindikwa siitwazo Mwage ambazo ni za
asili.
Mgoga hii aina ya Mlenda inapendwa sana na kabila la waruguru
kwa sababu inaleta sana hamu ya kula hasa hasa kwa wagonjwa na walio wazima.
Selina alisema kuwa mboga hiyo ikisha sindikwa huwa inasagwa
na kuchekechwa na kisha kuwa unga kabla ya kupikwa.
Alisem,a baada ya kuolewa mwaka 1983 hakuona sababu ya
kuendelea kukaa tu nyumba bila kujishughulisha, na ndipo alipo amua kuanza
kutafuta maisha yake ya kujitegemea.
Alisema kuwa kabla ya kupata mafunzo ya kutengeza sabuni na
batiki 1990, alianza na kazi ya kulima bustani za mbogamboga ili kujikimu
kimaisha.
Baada ya miaka saba ya ukulima ndipo serina alip[o jitosa
rasmi katika biashara ya kutengeneza batiki kwa kuanzia na mtaji wa shilingi
16,000.
Alisema kuwa kabla ya kuanza kutengeneza batiki alitumwa na
kanisa la Moravian ofisi ya wilaya mkoani Rukwa, iliyo kuwa chini ya uongozi wa
mchungaji Kibona na kamati yake kwenda kusomea utengenezaji wa batiki kwenye
jingo la mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Selina aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki mbili
ndipo alipo ludi rasmi kanisani , na kuanza kutoa mafunzo kwa akinamama,
wakinababa, na vijana wa madhehebu mbalimbali.
Anasema alifanya kazi hiyo kuanzia mwaka 1990 mpaka 2003 na ndipo walipo hamia
mkoani tabora, baada ya mumewake kupata uhamisho wa kikazi.
itaenedea kesho Uskose