Viongozi wa dunia wanaokutana kwenye Hadhara Kuu ya
Umoja wa Mataifa, leo watazingatia kampeni inayoongozwa
na Marekani kuwaangamiza wapiganaji wa Dola la Kiislamu
nchini Iraq na Syria na hatua za kuwapiga marufuku
wapiganaji wa kigeni.
Rais Barrack Obama (Pichani) wa Marekani anayetafuta uungaji
mkono wa kimataifa dhidi ya wapiganaji hao, ni miongoni
mwa viongozi wa kwanza watakaohutubia katika mjadala
huo wa Baraza Kuu, unaoanza leo.
Baadaye Obama atauongoza mkutano maalum wa Baraza
la Usalama, linalotazamiwa kupitisha azimio juu ya kuzuwia
wapiganaji wa kigeni kwenda Iraq na Syria. Kitisho cha
kundi hilo la Dola la Kiislamu kilisababisha Marekani
kufanya mashambulizi ya angani nchini Iraq mwezi uliopita,
na jana ikatanua kampeni yake hiyo na kuzishambulia
ngome zao nchini Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)