SHULE za msingi halmashauri ya wilaya ya Njombe zinaupungufu
wa madawati 2028, katika shule zake 52 zanye jumla ya madarasa zaidi ya 9000.
Hayo tamebainishw ana afisa elimu ya msingi halmashauri ya
Njombe, Hamis Milowe, wakati wa kupokea madawati 100 kutoka kwa Benki ya NMB
tawi la Njoimbe.
Milowe alisema kuwa katika shule za halmashauri hiyo kuna
madarasa 9125, ambapo kunahitajika kuwa na jumla ya madawati 6997 ambapo
kulikuwa na upungufu wa madawati 2128 na upungufu huo umepunguwa baada ya
kupokea madawati 100 na kubaki na uhitaji wa madawati 2028.
Alisema kuwa halimashauri imekuwa ikipigana kutafuta wadau
mbalimbali kuhakikisha wanapata madawati yatakayo kidhi mahitaji ya shule za
halmashauri hiyo na kuondokana na adha hiyo ya madawati.
Kwa Upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Paulo Malala
alisema kuwa Benki hiyo imekuwa ya Kwanza katika kutoa msaada wa kielimu kati
ya wadau walio fuatwa na halimashauri hiyo kuchangia upande wa madawati.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Njombe Shaibu Masasi alisema
kuwa kwa upande wa elimu kufikia malengo ya Matokeo Makubwa sasa (BRN) itakuwa
ni rahisi kama miundombinu ya madawati itapatikana na wanafunzi wakisoma katika
mazingira mazuri.
Alisema kwa kupata madawati wanafunzi wataweza kuifikisha
malengo ya BRN kwani wakikaa chini kusoma inakuwa ni tabu na kufanya vizuri ni
ndoto.
Hata hivyo afisa uhusiano nyanda za juu kusini wa Benki ya
NMB, Focus Lubende alisema kuwa madawati hayo yanathamani ya shilingi milioni 5
na huo mi moja ya kurejesha faida kwa wateja wake.
Alisem a kuwa Benki hiyo imetenga jumla ya Bilion 1 kwa ajili
ya kuchangia maendeleo kwa wananchi katika sekta ya afya na elimu.