Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Falls ameapa kwamba hakutakuwa
na majadiliano yoyote na kundi la Algeria linalofungamanishwa na
wanamgambo walio na itikadi kali wa dola la Kiislamu, lililokiri
kumteka nyara raia wa Ufaransa, na kusisitiza kuwa Ufaransa
itaendelea na mashambulizi yake ya angani dhidi ya kundi hilo. Kundi
hilo la Jund al-Khalifa au wanajeshi wa utawala wa sheria za
kiislamu, wameahidi katika ujumbe wao kwa njia ya Video kwamba
watamuua mateka huyo Herve Pierre Gourdel, saa 24 zijazo ikiwa
Ufaransa haitositisha mashambulizi yake dhidi ya kundi la IS nchini
Iraq. Ijumaa iliopita Ufaransa ilifanya shambulizi lake la kwanza la
angani nchini Iraq lakini ikasema haitofanya mashambulizi kama hayo
nchini Syria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)