Marekani na washirika wake wa kiarabu wameanzisha mashambulizi
kutoka angani na baharini dhidi ya wanamgambo walio na itikadi kali
wa Dola la Kiislamu IS nchini Syria, na kufungua mkabala mpya
katika vita dhidi ya kundi hilo la kikatili la wapiganaji wa jihadi.
Uongozi wa juu wa jeshi la Marekani umesema nchi za Bahrain,
Jordan, Saudi Arabia, Qatar na nchi ya falme za kiarabu zimeungana
na Marekani katika mashambulizi hayo. Mashambulizi hayo
yaliyaharibu au kuviangamiza vituo vingi vilivyolengwa vya
wapiganaji hao katika ngome zao Kaskazini mwa Syria na karibu na
mpaka wa Iraq , yakiwemo maeneo ya mafunzo, taasisi za
mawasiliano na magari ya kivita. Mashambulizi ya angani
yanayoongozwa na Marekani nchini Syria yameleta sura mpya
katika vita vyake dhidi ya wanamgambo wa IS wanaodhibiti maeneo
mengi nchini Iraq na Syria na kutangaza utawala wa sheria ya
kiislamu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)