Mkutano mkubwa wa viongozi duniani kuhusu mabadiliko ya tabia
nchi unafunguliwa leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini
New York Marekani, huku kukiwa na wito wa kupunguza hali ya joto
duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ndiye
mwenyeji wa mkutano huo atakayewaongoza viongozi takriban 120,
huu ukiwa mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu tokea ule
uliofanyika
Copenhagen mwaka wa 2009
na kumalizika bila ya mafikiano.
Wanadiplomasia na wanaharakati wa mabadiliko ya tabia nchi
wanauona mkutano huu kuwa muhimu na kuelekea mkutano
mwengine uliopangwa kufanyika mjini Paris mwishoni mwa mwaka
wa 2015 ambao unatarajiwa kuweka mipango ya kupunguza utoaji
wa gesi chafu inayoharibu mazingira,baada ya mwaka 2020.
Habari Online na Elimtaa
Israel kuishawishi Marekani
Mkutano wa mabadiliko ya hewa waanza hii leo Marekani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)