Wadau wa Michezo Zanzibar Wapitia Rasimu ya Michezo 2014

Wadau wa Vyama vya michezo na vilabu mbalimbali Zanzibar wakipitia Rasimu ya Michezo ya mwaka 2014 kwa kuijadili na kuifanyia mapitio ile ya Sera ya Taifa ya Michezo ya mwaka 2007, ambayo inaonekana haikidhi haja na mahitaji ya maendeleo ya michezo Zanzibar kitaifa na kimataifa, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Sanaa rahaleo na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michechezo Ndg. Issa Mlingoti.  
Na kushirikisha Vyama vyote vya michezo Zanzibar na Vilabu mbalimbali vya michezo yote Zanzibar.
Wadau wa Vyama vya michezo vya Watu wenye Ulemavu Zanzibar wakipitia Rasimu ya Michezo ya mwaka 2014 kwa kuijadili na kuifanyia mapitio ile ya Sera ya Taifa ya Michezo ya mwaka 2007, ambayo inaonekana haikidhi haja na mahitaji ya maendeleo ya michezo Zanzibar kitaifa na kimataifa, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Sanaa rahaleo na kufunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michechezo Ndg. Issa Mlingoti.
Wadau wa Michezo Zanzibar wakipitia na kujadili rasimu ya michezo ili kuiboresha zaidi kimataifa na kukidhi haja ya wanamichezo na Taifa.
        Wadau Mchezo wa Riadhaa wakiwa katika makundi kujadiliana rasimu hiyo katika ukumbi wa sanaa raheleo 

Wadau wa michezo kutoka Vyama vya ZFA na BMZ  wakipitia rasimu vifungu hadi vifungu kupitisha na kuchangia rasimu hiyo ili kuiboresha zaidi.kuleta mafanikio na kukuza michezo Zanzibar kimataifa na Kitaifa kurudisha hadhi yake Zanzibar katika sekta ya michezo.
Wadau wa sanaa ya Usanii Zanzibar wakipitia rasimi hiyo kuiboresha zaidi kukuza kiwango cha michezo Zanzibar.
Wadau wa michezo wa Vilabu vya mchezo wa mpira wakipitia rasimu hiyo, katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.