Kerry azungumzia kitisho cha wa wanamgambo wa IS na Iran
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amekuwa na mazungumzo na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif juu ya kitisho cha wanamgambo walio na itikadi kali wa dola la kiislamu nchini Iraq na Syria, mazungumzo yaliofanyika mjini New York Marekani. Mawaziri hao wawili walikutana kwa zaidi ya saa moja jana katika hoteli moja mjini humo na kuzungumzia hatua zilizopigwa katika majadiliano, juu ya nyuklia na pia kuzungumzia kitisho cha wanamgambo wa ISIL. Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani, amesema Iran ina mchango wa kutoa wakati Marekani ikitafuta kuunda muungano wa kupambana na wapiganaji wa jihadi wanaodhibiti sehemu kadhaa nchini Iraq na Syria.