Wanavyuo kuanza kuburudishwa na Bendi Mjidi Dodoma

Kwa Kiingereza Bofya hapa


 Waimbaji wa Bend ya HRB
 Mpiga Ngoma wa HRB,



 Kiongozi wa Bendi ya Hitman redemption Band ya Dodoma, James Mwampona



 Mchingaji wa kanisa la Pendecost Ihumwe.

WANAVYUO mbalimbali Mkoani Dodoma wanatarajiwa kuanza kuburudika kwa nyimbo za injiri usiku kwazamu wakati wale wasio abudu wakielekea katika kumbi za Starehe.
Akizungumza na Elimta kiongozi wa Bendi mpya ya nyimbo za Injili Hitman Redemption Band, ya Mjini hapa, mda mfupi baada ya Ibada ya sifa katika kanisa la Pendecost Ihumwe, James Mwampona alisema kuwa kuanzishwa kwa bend hiyo kunalenga kuwaburudisha wakazi wa Mkoani hapo ikiwa ni pamoja na wanavyuo waumini.

Alisema kuwa bend hiyo ni mpya kwa mkoani Dodoma na inaundwa na wakazi watu kutoka katika makanisa mbalimbali na hutoa huduma pale itakapo hitajika.

“Bend hii inaundwa na watu kutoka katika makanisa mbalimbali na ipo tayari kutoa huduma ya uimbaji pale itakapo hitajika bila kujali ni kanisa gani,” Alisema Mwampona.

Na kuongeza “Bend hii itavunja upweke katika vyuo hapa mjini Dodoma wakati wengine wana enda kwenye kumbi za usiku sisi tutakuwa tukienda katika kumbi sha shule na kutoa huduma hapo ili tu kuweka burudani kwa wanavyuo ambao hawana uwezo wa kwenda disco.”

Alisema bendi hiyo kwa sasa ipo katika ziara katika makanisa mbalimbali katika mkoa wa Dodoma na kutoa huduma katika makanisa hayo baada ya ibada kutoa huduma ya uimbaji wa sifa na njimbo za kuabudu.

Alisema kuwa lengo la kufanya ziara hizo katika makanisa mbalimbali ni kuhakikisha kuw ahuduma ya uimbaji ina samba katika kila kona na watu kuburudika kupitia uimbaji.

Mwampona, ambaye pia ni muimbaji katika bendi hiyo alisema kuwa bend hiyo ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa Mjini Kigoma na baada ya kuhudumu kwa muda kidogo bendi hiyo imehamia mkoani homu kwaajili kutoa huduma.