Kwa Kiingereza Bofya hapa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais uratibu
na Mahusiano Sephen Wassira, amesema kuwa katika katiba mpya kunatarajiwa
kuwekwa kipengele kitakacho iweka ardhi kisheria na kutambulika kama rasilimali
ya taifa.
Akizungumza katika maonyesho ya
Nanenane baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika viwanya Vya maonyesho
hayo vya Nzuguni mjini hapa, Wassira ambaye ni mwenyekiti wa moja ya kamati za
bunge la katiba, alisema kuwa katika katiba hii kumejadiliwa kibengele
kitakacho ilenga ardhi na kuwema mamlaka zitakazo simamia moja kwa moja.
Alisema kuwa itakuwa hivyo kwa
sababu ardhi ndio msingi wa maisha ya mtanzania kwani maliasili zote zipo ndani
ya ardhi.
“Shabaha ni kuweka katika sura ili
katiba ielekeze mamlaka zitakazo simamia juu ya namna rasilimali za taifa
zitakavyo simamiwa kama vile gesi, Ardhi na maliasili zingine zilizopo chini ya
ardhi, Alisema Wassira.
Alisema kuwa bunge hili kabra halija
malizika linatarajia kushugulikia mambo hayo kabla halijamalizika kuhakikisha
kuna kuwepo kwa sura hiyo katika katiba mpya.
Alisema kuwa jambo hilo litakuwa ni
hakikisho kwa wakulima kwani ardhi itapata msimamizi mwenye nguvu na kuipa
ardhi umuhimu wa hali ya juu kuliko ilivyo hivi sasa.
Aidha Wassira alisema kuwa yeye kama
Mwenyekiti wa kamati namba sita kamati yake mpaka sasa imejadili sura tatu na
kuwa ilitakiwa kufika juma tatu wawe wajadili sura nne.
Hivyo katika kamati yake katika
kamati yake ambayo juma tatu inaanza sura ya nne, alizitaja sura ambazo tayari
zimejadiliwa katika kamati yake kuwa ni pamoja na sura inayo husu sera za jumla
za taifa ambazo zitakuwa ni msingi wa kutengeneza sera na sheria za nchi.
Alisema mbali sura hiyo pia
wamejadili sura ya Tatu ambayo inazungunzia maadili na miiko ya viongozi
itakayo wazibiti wanao penda kutafuna mali za wananchi.
“Kumekuwa na baadhi ya watu
wakipatiwa nafasi ya uongozi wamekuwa wakiwaza kutafuna mali za wananchi na
badala ya kuwaza wataiingizia nchi nini katika uongozi wao, katika majandiliano
yetu tumeweka vifungu katika katiba vitakavyo wabana watu wanao tumia vibaya
rasilimali za taifa,” Alisema Wassira
Kuhusiana na wajumbe kuingia walio
toka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Wassira amesema kuwa katika kamati
yake hawajapokea mgeni yeyote kutoka nje ya walio ingea ile siku ya kwanza.
Alisema kuwa yeye hana shida na
wajumbe hao na waendelee kurejea katika bunge hiro na nibusara kurudi katika
bunge hilo ni jambo la busara.
“Naona ni busara kuendelea kurudi
katika Bunge ra katiba kwani naona wanavyo fanya wale wanao wakemea wale
wanaonaoendele kuingia katiba bunge la Katiba,” Aliongeza Wassira.