Kwa Kiingereza Bofya hapa
Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero
lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika
wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe
la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti
20, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa
furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi
la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014.
Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri
(kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete
(nyuma ya Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa
baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto
Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John
Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani
(kulia), Mbunge wa Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga
Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul
Mteketa (kulia kwa Rais)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu
ya ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014.
Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama
Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada
ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto
Kilombero wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe
la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero wilayani
Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014 (Picha na Ikulu)