Mtaala wa masomo ya Vyakula na lishe yarudushwe


Kwa Kiingereza Bofya Hapa
SERIKALI inatakiwa kurudisha mitaala ya maarifa ya nyumbani katika shule za Msingi ili kuzuia tatizo la kudumaa unaoikabili jamii ya kitanzania kutokana na elimu mpangilio wa Chakula na lishe kuwapo majumbani.

Wakizungumza wakati wa kuwasilishwa sera ya Chakula na Lishe Mjini hapa baadhi ya wabunge waliohuzuria katika mkutano huo walisema somo la Maarifa ya nyumbani lirudishwe shuleni ili wanafuzi wafundishwe masuala hayo wakiwa shuleni.

Akichangia katika mkutano huo Mbunge wa viti maalim Mbeya (CCM) Hilda Ngoye, alisema kuwa somo la chakula na lishe lirudishe katika shule za msingi ili wanafunzi wajifunze wakiwa mashuleni.

Somo hilo ni lazima liludi mashuleni na kuwa watu wa zamani walikuwa na akili kutokana na kupangilia chakula kutokana na mtaala huo kuwepo mashuleni watoto walikuwa wanafundishwa wakiwa mashuleni.

Alisema kuwa kunatakwimu zimetolewa hivi karibuni zikisama kuwa asilimia kubwa ya watoto wa Tanzania wanaudumavu wa akili kutokan ana ukosefu wa lishe.

Ngoye alisema kuwa serikali toka ilipo ondoa somo la Maalifa ya Nyumbani watoto wamedumaa akili kutokana na kula mlo wa aina moja pekee na kutoka baadhi ya virutubisho.

“Zamani tulikuwa na somo la Domestic Science ambalo lilitusaidia katika masuala ya upangaji wa chakula katika tukifika nyumbani la kuwafundisha wazazi wetu, si unaona miili ya sisi wazee wa zamani miili yetu ilivyo tulikuwa tunakula chakula kilicho kamili,” Alisema Ngoye.
  
Wabunge hao waitaka serikali kurudisha somo hilo kuanzia shule ya awali ili wanafunzi wajengeke kuanzia wakiwa wadogo kuhusiana na masuala ya lishe.

mtaala wa masomo ya chakula lazima ulidi shule za msingi