WANAWAKE WATAKIWA KUUNDA MAKUNDI ILI KUKOPESHEKA


WANAWAKE nchini wametakiwa kuunda makundi madogomadogo ili kuweza kukopesheka fedha kutoka kwa taasisi za kifedha na pesa zinazo tolewa na serikali ili kuanzisha miradi yao itakato wawezesha kuendesha maisha yao na kuacha utegemezi kutoka kwa waume zao.
Wengi wao wamekuwa wakishindwa kutumia fulsa za kupata mikopo mbalimbali kutokana na kwenda kufuata mikopo wakiwa mmoja mmoja na taasisi za kifedha kushindwa kuwapa mikopo.

Akizungumza katika harambee ya kukuza mfuko wa kikundi cha Chawakido mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Dodoma,Anton Mavunde alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuunda makundi yatakayo wawezesha kupata pesa watakapo hitaji mkopo kutoka katika taasisi za kifedha.

Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakishindwa kupata msaada wa kukopeshwa pesa kutokana na wanawake kuto kuwa katika makundi ambayo taasisi hizo zinahitaji yawepo ili kukopeshwa fedha.

Mapunda alisema kuna fedha ambazo huwa zinatolewa na serikali kwaajili ya makundi ya kijasiliamali kukopeshwa kwa masharti nafuu lakini makundi yamekuwa ni machache na walio katika makundi wananufaika na mikopo hiyo.

Ametoa wito kwa wanawake kwa wanaumekuunda makundi yatakayo wasaidia kutambulika katika taasisi za kifedha na kupata mikopo yenye masharti nafuu na kuendeleza miradi yao na kuboresha maisha yao.

Katika harambee hiyo mgeni rasimi, Salome Kiwaya alitoa shilingi Ml 1 kwa kikundi hicho na kuwataka wanawake hao kuachana na mambo ya Umbea umbea ili kusonga mbele na kufanya shughuli za kimaendeleo.

Alisema wanawake wengi wanashindwa kufanya maendeleo kutokana na muda wao mwingi kutumia katika kufanya umbea na shughuri za kimaendeleo kukwama.

Kiwaya alisema kuwa wanawake hao wa nia waliokuwa nayo watafika na wajitahidi kuudumisha umoja wao na kuhakikisha hakuna mtu anaye haribu umoja wao na wasonge mbele kimaendeleo na kuwa mfano wa kuighwa.

Wasikoma risara yao wanawake hao walisema kuwa wamejitahidi kufanya shughuli zao na kufikisha Sh. Mil 5 na wanauhitaji wa kuwa na milioni 12 zitakazo waondolea changamoto zao walizonazo kwa wakati huu.