MRADI WA MADINI WATEMBELEWA


Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma kutoka kwa Meneja Utawala Msaidizi wa kampuni ya Tanzania – China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) Bw. Israel Mkojera. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Mlingi E. Mkucha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama wa NDC Bw. Ramson Mwilangali (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (wa pili kushoto), Erasmus Masumbuko, Tume ya Mipango (wa tatu Kushoto). 
 Viongozi pamoja na Maofisa kutoka Tume ya Mipango wakiangalia sehemu ambayo makaa ya mawe yanaonekana juu ya ardhi. Kulia ni mhandisi wa madini kutoka kampuni ya TCIMRL. Kampuni hii ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania, na kampuni ya Sichuang Hongda Group Limited ya China. 
 Sehemu ambayo makaa ya mawe yanaoneka kwa juu katika uhalisia wake.
Shimo hili lilichimbwa mwaka 1956 kwa ajili ya utafiti kuangalia tabaka za makaa ya mawe katika eneo hilo la Mchuchuma.