MALECELA AKABIZIWA KIPIGIA MTAMA

WAZIRI Mkuu mstaafu John Samwel Malecela, amewashauri wakulima wa mkoa wa Dodoma kutumia mashine za kisasa katika kupiga zao la mtama mara baada ya kuvuna ili kusaidia kuwa na ubora.
 
Malecela amesema hayo wakati akipokea mashine ya kupiga mtama iliyotengenewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini Sido.

Amesema kuwa wakulima wengi mkoani hapa wamekuwa na tabia ya kutumia zana za kienyeji katika kupiga zao hilo la mtama hali ambayo inasababisha kwa kiasi kikubwa kupungua kwa ubora.

Amesema kuwa kama wakulima watabadilika na kuanza kutumia zana za kisasa katika kupiga mtama watasaidia katika kuongeza thamani ya zao hilo na kusaidia kupata bei nzuri na soko la uhakika.