Haya ni matokeo kwa waliopiga kura ya kupendekeza muundo wa serikali tatu |
KATIKA uchangiaji na kutoa maoni katika rasimu ya katiba
Mpya wananchi wametakiwa kutoingiza itikadi za kisiasa wakati wa kuchangia.
Akifungua baraza la Katiba lililoandaliwa na Asasi ya Hope
for Deprived Action in Deveropment (HDPAD) ya Mji mdogo wa Mbalizi jana Afisa
Mtendaji wa Kata ya Usongwe, halmashauri ya Mbeya, John Mwanapazi alisema kuwa
wajumbe katika katiba hilo wasionyeshe itikadi yoyote.
Alisema kuwa wanao changia katika baraza hilo wasipinge kile
kilichopo katika Rasimu hiyo kwa kuonyesha itikadi ya aina yoyote iwe ya kidini
ama kisiasa.
“Katiba hii ni ya Tanzania sio ya kanisa ama dini yeyote na
sio katiba ya chama chochote cha kisiasa maoni yako yasiwe kamelenga katika
chama Fulani au kanisa unalotokea,” Alisema Mwanapazi
Aliongeza Katiba hii siyo ya Chadema, CCM wala CUF katiba
hii ni yawatanzania wote ya kizazi cha sasa na kijacho.
Alisema kuwa katika mapitio hao wasije wakaingiza chuki
binafsi kwa kuwa watu wanaugomvi wao wakapingana katika maoni yao.
Aliongeza kuwa katika maoni yao waangalie kuwa wanatoa maoni
ambayo ni ya taifa na sio ya kwao binafsi na kulenga kila kona ya nchi yetu.
“Ndugu washiriki hakikisheni maoni unayo yatoa yawe
yamelenga katika mrengo wa kitaifa zaidi na sio kuangalia kwa upanda wa
kikata,” Alisema Mwanapazi