MTOTO WA DARAZA LA PILI AFARIKI DUNIA




MTOTO Pasto Furaha (11) mwanafuzi wa daraza la pili, mkazi wa kijiji cha Mapinduka kata ya Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kugongwa na lori.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Diwani Athumani alisema kuwa mtoto huyo aligongwa na roli hilo Juzi majira ya 12:30 jioni katika maeneo ya Mwapimbuka barabara ya Mbeya- Iruinga mkoani Mbeya.

Alisema Marehemu huyo alifariki wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Igurusi na mwili wake umehifadhiwa kituoni hapo.

Alisema kuwa mtoto huyo alikuwa mwanafunzi wa daraza la Pili katika shule ya msingi Igurusi ya wilayani humo.

Athumani alisema kuwa gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Habibu Hassan (28) likiwa na namba za usajili T 877 CLX na trela namba T 242 CLV aina na Iveco.

Alisema kuwa gari hiyo inashikiliwa na Polisi na lipo katika kituo cha polisi cha kata ya Igurusi.

Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwengo kasi wa dereva wa roli hilo la mizigo na akasababisha ajali hiyo.
Athumani alisema kuwa jeshi la Polisi linatoa wito kwa watumiaji wa barabara kuwa makini na madereva kuwajali watembea kwa miguu.