WIZI wa pikipiki na mifugo umeongezaka kwa kasi kwa
kipindi cha mwaka jana kuliko makosa mengine ya uhalifu jijini Mbeya kwa
asilimia 103 na 18 .
Akitoa taarifa ya kufunga mwaka Kamanda wa polisi mkoa wa
Mbeya diwani athumani alisema kuwa kwamwaka unao isha makosa ya wizi wa
pikipiki na wa mifugo yameongezeka kwa kwa asilimia kubwa ulikinganisha na
makosa mengine ya uhalifu ambayo yamehuka.
Alisema kuwa kwa kuwanza na wizi wa pikipiki kwa mwaka
juzi makosa hayo yalikuwa 56 na kwa mwaka jana yameongezaka na kifikia makosa
114 ambayo ni sawa na asilimia 103.
Makosa hayo yamelipotiwa katika vituo vya polisi katika
maeneo mbalimbali mkoani hapa ambapo kwa mwaka jeshi hilo litajitahidi
kuhakikisha linapunguza.
Akizungumzia wizi wa mifugo Athumani alisema kuwa makosa
ya wizi huo yameongezeka kwa asilimia 18 ambapo kwa mwaka jana yalilipotiwa
makosa 196 na hadi kufikia Novemba mwaka jana kumekuwa na ongezeko la makosa
hayo hadi kufikia 233.
Alisema kuongezeka kwa makosa hayo ya uhalifu kunatokana
na juhudi zinazo fanywa na jeshi hilo kwa kusjhirikiana na wadau mbalimbali
wakiwemo na wananchi.
Mbali ya kuonezeka kwa makosa hayo pia jeshi la polisi
kwa mwaka jana limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na silaha
20 kati ya siraha hizo ni pamoja na magobole 16 Smg mbili Riffle moja, S/gun
moja na risasi 190.
Athumani aliongeza kuwa pia wamefanikiwa kuwakamata
wahamiaji haramu 535 kutoka katika nchi za Ethiopia, Somalia, Kenya, Malawi na
DRC Congo.
Alivitaja vitu vingine vilivyo kamatwa kuwa ni pamoja na
Noti bandia 292, zenye thamani ya Tsh 2,160,000/= madawa ya kulevya, mafuta ya
wizi aina ya diesel lita 5,855, bidhaa za magendo zenye thamani ya Tsh. 9,
800,000, mifuko 45 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa barabara.
alisema kuwa kwamwaka huu watajitahidi kushirikiana na
wananchi ili kupambana na matukio mbalimbali yanayo tokea katika jamii na
kuiomba jamii kutoa taarifa mapema endapo wanahisi kutokea kwa uharifu wowote.