WATU WAKAMATWA NI KUTOKA ETHIOPIA

JESHI la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu watatu raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali katika maeneo ya Uyole jijini Mbeya. Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya jana Kamanda wa polisi Mbeya Diwani Athumani alisema kuwa askali waliokuwa doria waliwakamata watu watatu raia wa Ethiopia walioingia nchini bila kibari. Alisema kuwa watu hao walikamatwa katika maeneo ya Uyole majira ya saa 1:30 jioni wakiwa wanateremka katika basi la El Saidy. Athumani alisema watu hao walikuwa wanashuka katika basin a hatimaye wakakamatwa na askali waliokuwa katika dolia maeneo hayo ya Uyole jijini Mbeya. Aliwataja raia hao wa kisomalia kuwa ni Desta Bermamu, (22), Temesgen Yosef, (20) na Maharatu Tamasce, (22) ambao walikuwa wametokea Nchini kwao. Aidha alisema kuwa hatua za kisheria zitafuata juu ya watuhumiwa hao na kuwakabidhi wa maafisa uhamiaji mkoa wa Mbeya. Hivyo alitoa wito kwa wanajamii kuendelea kutoa ushirikiano na kuonyesha jitihada za kuwakamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya kuingia nchini bila ya kibali. Aliwataka watanzania kwaujumla na hasa wale wamipakani kutoa taarifa mapema kwa jeshi la polisi kama wanahisi kuwapo kwa wahamiaji halamu katika maeneo yao haraka hii isasaidia kuwakamata mapema.