MPANDA BAISKELI AGONGWA NA IT

MPANDA baiskeli mkazi wa Mbalizi wilayani Mbeya mkoani hapa amefariki papo hapo baada ya kugongwa na lori liendalo nje ya nchi maeneo ya Mbalizi. Gari hiyo iliyokuwa kasi na ikisafirishwa kutoka badalini kwenda nje ya nchi lilingonga mpanda baiskeli Hassan Patrick mkazi wa Mbalizi na kufa hapo hapo. Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alisema kuwa gari hiyo yenye namba za usajiri IT 2572 aina ya Isuzu lori likiwa kasi lilisababisha kifo cha mkazi huyo juzi majira ya saa 2:00 asubuhi. Alisema lori hilo lilikuwa kikiendeshwa na Kunda Antin (39) mkazi wa Chingola nchini Zambia, na lipo katika kituo cha polisi. Athumani alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali teule ya Ifisi ya wilaya Mbeya mkoani hapa. Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni mwendokasi wa lori hilo ambapo lili acha njia na kumvaa mpanda baiskeli.