KILA OFISI KUNA UMUHIMU WA WATU WENYE ELIMU YA CHINI
SERIKALI licha ya kuwa na dhamila ya kuzipa hadhi taasisi za sayansi na teknolojia kuwa vyuo vikuu isiwe sababu ya kuwasahau Mafundi mchundo katika suala zima la utendaji wa kazi.
Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya utendaji wa kazi katika sekta yoyote ile mfanyakazi mkubwa ni yule mwenye elimu yachini na maranyingi watu wenye elimu ya juu huwa ni watekelezaji tu.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba katika mahafali ya saba ya Taasisi ya Sayansi na Teknolokia Mbeya (MIST) yaliyo fanyika mwishoni mwa wiki iliyopiya chuoni hapo alisema katika ofisi yoyote ile wafanyakazi wenye elimu ya chini ndio wanaofanya kazi kubwa.
Makamba alisema kuwa chuo hicho ambacho kwa sasa bado ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, hivi punde itapewa hadhi ya kuwa chuo kikuu, hivyo kufuatia hali hiyo isiwe kigezo cha kuanza kuzalau mafundi mchundo maana haiwezekani kila mtu kuwa Injinia.
Hata hivyo alisema serikali haina maana kuwa kuanzisha vyuo vikuu ni sababu ya kutatoa watu wenye elimu ya juu pekee, bali hata ngazi ya cheti na diproma lazima wawepo ili kuleta uwiano wa kazi.
“Nipende kuwambia kwamba wote tukiwa Mainjia hapa hatuwezi kufanya kazi, ikumbukwe kuwa wafanyazi wa kubwa ni wale mafundi Mchundo ambao wanatumwa kupigilia misumali juu ya nyumba kwa hiyo tukifanya kuwapoteza hawa itakula kwetu,” alisema Makamba.
Aidha Naibu waziri, alisema kuwa lengo la serikali ni kuendeleza chuo hicho ili kiwe chachu ya kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu nchini.
Alisema kuwa takwimu za udahili wa wanafunzi katika fani za sayansi na teknilojia katika vyuo vingi hapa nchini siyo za kuridhisha, na pia udahili wa wanafunzi wa kike bado ni wa kiwango cha chini sana.
Hivyo alisema pamoja na juhudi kubwa zitakazo elekezwa katika udahili ni vyema kuhakikisha ongezeko la udahili wa wanafunzi unaendana na viwango bora vya elimu inayotolewa na kuwajengea uwezo mzuri wahadhiri.
Naye Mkuu wa chuo hicho Profesa Joseph Msambichaka alisema kuwa anatoa shukurani zake za dhati kwa Rais Jakaya Kikwete kutimiza vigezo vya kupandisha chuo hicho kuwa chuo kikuu kabla ya mwaka 2015 kama ilivyo pangwa kukamilika.
Katika mahafali hayo wanafunzi 328 walitunukiwa vyeti katika fani mbalimbali, ambapo kati yao wahitimu 124 katika ngazi ya Stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma) na wahitumu 204 katika ngazi ya Shahada ya kwanza.