CHUNYA: RISASI 114 ZA SMG ZAOKOTWA POLINI

ASKALI mgambo wa Bitmanyanga wilayani chunya wameokota risasi za SMG 114 katika hifadhi Lukwati iliyopo kijijini hapo wakati wakiwa dolia ya kudhibiti majangili. Mgambo hao waliziokota silaha hizo mwishoni wa wiki iliyopika ambapo zilitelekezwa zikiwa katika mfuko na mtu asiye fahamia ambaye walimuonda kwa mbali. Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya juzi kamanda wa polisi mkoa mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alisema risasi hizo ziliokotwa katika poli la hifadhi ya Lukwati iliyopo katika kijiji cha Bitimanyanga wilayani Chunya. Alisema kuwa risasi 114 za SMG ziliokotwa na askali wa Mgambo aliyefahamika kwa jina la Daimon John (32) mkazi wa Bitimanyaga akiwa na wenzake waliokola risasi hizo. Athumani alisema kuwa risasi hizo zilikutwa zikiwa katika mfuko na katika mfuko huo pia kulikuwa na Radio nguo vyote vikiwa vimetelekezwa. Alisema kuwa mbinu iliyo tumika kuutelekewa mfuko huo ni baada ya kuwaona askali jangili huo na kutokomea katika poli moja katika hifadhi hiyo. Hivyo ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa Mkoa wa mbeya kuachana na kufanya kazi zisizo haralai na kufanya kazi ambazo zinakubalika katika jimii na watafanya kwa amani.