HAKUNA
binadau aliyezaliwa kuwa fukala wala tajiri bali juhudi na uvivu ndivyo
vinasababisha mtu kuwa katika hali nzuri au mbaya katika maisha.
Hayo yamebainishwa
juzi jijini Mbeya na mkurugezi wa shirika la Nyumba la taifa, Nehemia Mchechu ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 50 toka kuanzishwa kwa shule ya
sekondari Mbeya Day ya jijini hapa.
Alisema kumekuwa
na tabia ya watanzania wengi wanao jijegea mawazo kuwa wao ni maskini na mawazo
yao kuwa halisi katika maisha yao.
“Watanzania
wengi wanakuwa wasikini kwa kujitakia kwani wamekuwa wakijidharau na
kujibweteka pasipo kujishughulisha na hatimaye kutegemea serikali iwafanyie
kitu ili kujikwamua katika maisha yao,” alisema Mchechu.
Aliwataka
wanafuzi wa shule huyo kuwa makini wanapojisomea na kujijengea kuwa wanataka
kuwa wakina nani hapo watakapo hitimu elimu zao na hii itamfanya mwanafuzi
kufikia mareko na kujiweka katika nafasi mzuri.
Alisema kumekuwa
na wanafunzi wanao soma ilimradi tu katimiza wajibu wa kwenda shule na kujikuta
wanahitimu kwa kupata pasi zisizo za kurizisha hii inatokana na kuto kuwa na malengo
wanapo kuwa shuleni.
Katika maadhimisho
hayo ya miaka 50 yaliambatana na halambee ya kuchangia ukarabati wa maabara ya
shule hiyo ambayo imefanikiwa kutoa baadhi ya watu maarufu wenye nyadhifa
tofauti.
Mmoja wa
watu waloatoka katika shule hiyo ni pamoja na Nehemia Mchechu, Mh. Joseph Mbilinyi
(Sugu) mbunge ya jimbo la Mbeya Mjini, Naibu waziri wa elimu, Philipo Mlugo hao
ni baadhi tu ya watu walohitimu katika shule hiyo katika miaka yake 50.
Katika halambee
hiyo shule ilifanikiwa kupata zaidi ya milioni 60 ambapo walikuwa na lengo la
kupata millioni 150 kwaajili ya ukarabati wa maabara ya shule hiyo na nyumba ya
mwalimu.
Mchechu
alitoa wito kwa wanafunzi washule hiyo kuwa wamalizapo wakumbuke kurudi katika
shule yao na kuwataka wale walio hitimu katika shule hiyo kwa miaka ya hapo
nyuma kujitokeza na kujitolea kwaajili ya shule yao.