UTAFITI wa majaribio ya chanjo ya VVU hivi katibuni
unatarajia kuingia katika hatua ya mwezi huu utakao fanyika katika mikoa miwili
kwa Tanzania na moja katika nchi ya Msumbiji ambao unafahamika kwa jina la TaMoVac
02 baada ya kumaliza ule wa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utafiti huo
mpya wa hatua ya pili ya majalibio ya chanjo hiyo, mtafiti mkuu wa kituo cha
utafitu mkoani Mbeya cha NIMR-Mbeya Dkt. Lenard Maboko amsema kuwa utafiti huo
utakuwa katika majalibio ya pili ya chanjo ya VVU.
Aliitaja vituo vitatu vitakavyo husika na utafiti huo kuwa
ni Mbeya, Dar es salaam kwa Tanzania na Maputo kwa Msumbiji ambapo utaendeshwa kwa muda wa miaka miwili.
Alisema kuwa utafitu huu utachukua washiriki 80 kwa jiji la
Dar es salaam washiliki 80 Mbeya na washiliki 38 kwa Maputo Msumbiji huku
utafiti huu ukiwa umebuniwa kuhakikisha usalama wa mchanganyiko chanjo na
kutambuaaina za witikio wa kinga zinazosisimua mwili.
Washiriki 120 Tanzania na washiriki 24 Msumbiji ambao
walipatiwa mchanganyiko wa chanjo kama hizi katika utafiti wa kwanza TAMoVac 01
na kuonekana kuwa chanjo hizi zinastahimilika vizuri.
Dkt. Maboko alisema kuwa kituo cha utafiti wa magonjwa ya
binadamu Mbeya NIMR-Mbeya inafanya
utafitu huo na pia utafanyika katika chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi
Muhimbili, Dar es salaam pamoja na Maputo Msumbiji katika taasisi ya afya ya
taifa Nchini humo.
Alisema kuwa njia hiyo imebuniwa kutoa chanjo ya VVU na
imebuniwa kukinga aina mbalimbaliza virusi hivyo ambapo kutakuwa na chanjo ya
msingi ya vinasaba (DNA) kipigajeki chanjo ya kirusi cha vaccinia
kilichopunguzwa nguvu inachojulikana kama (MVA-CMDR) kwa pamoja zimetengenezwa
kutoamchanganyiko tofautiwa antjeni za VVU za aina ya A, B, C, D na E.
Alitaja kitu kipya na cha pekee katika utafiti huo kuwa ni
jinsi ambavyo moja ya chanjo hizo inavyotolewa chanjo ya vinasaba DNA ambazo
zinafaida nyingi na huku wa tafiti bado wanajaribu kugundua njia njia bora ya
kusitoa katika mwili wa binadamu ili ziwe na ufanisi mkubwa.