WANAFUNZI wa sule ya
msingi Ifumbo ya wilayani chunya ameokota bastora wakati wakicheza mpira katika
uwanja wa shule hiyo ikiwa na risasi moja.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alisema kuwa wanafuzi hao waliogota bastola
hiyo inayotumia risasi za S/Gun
ikiwa na risasi moja ya aina hiyo.
Alisema kuwa
siraha hiyo iliokotwa na wanafuzi wa shule ya msingi Ifumbo iliyopo katika kata
ya Ifumbo wilayani Chunya ambapo ilikuwa ni majira ya saa 3:00 asubuhi ambapo
waliokota bastola ikiwa katika Rambo.
Athumani
alisema kuwa siraha hiyo ilikuwa imeterekezwa katika pembezoni mwa kiwanja
hicho cha mpira na kuhifadhiwa ndani ya mfuko wa Rambo na kuokotwa na wanafunzi
hao.
Alisema kuwa
kitendo cha kumiliki silaha kinyume cha sheria ni kosa la jinai na endapo
mtuyeyote atakaye kamatwa atafikishwa katika vyombo vya sheria.
Pia ametoa
wito kwa wananchi na hasa kwa wakazi wa wilaya ya Chunya kuwa makini na umiliki
wa silaha kinyume cha sheria.