WADAU WSJITOKEZE KUSAIDI ELIMU




SERIKARI na wadau wa elimu za afya wanatakiwa kuatazama kwa jicho la pili katika taasisi mbalimbali za binafsi zinazo jihusisha wa utoaji wa elimu ya hiyo.

Taasisi hizo za binafsi zimekuwa zikijitahidi katika kuzalisha wauguzi wa afya na kukwama uendashaji wake kutokana na kuto kuwapo kwa ruzuku kwaajili ya kuendeshea taasisi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Afisa Mtendaji wa chuo cha St. John Helth college, Richard Mkwela cha jijini Mbeya, alisema kuwa vyuo vya binafsi vinakabiliwa na chamgamoto mbalimbali katika uendeshaji wa taasisi hizo hasa za kifedha.

Alisema kuwa wadau wanao jihusisha na kutoa ruzuku katika taasisi mbalimbali za kielimu hasa wanaotoa misaada na kuwa mamoyo wa kujitolea katika sekta ya afya.

Alisema kuwa kama wadau wanaojitolea katika elimu wajitolee katika suala la vyuo binafsi vya elimu ya afya na itasaidia kuboresha sekahiyo kama wanavyo jitolea katika sekta zingine za kielimu.

Mkwela aliitaka serikali kujitahidi kutoa ruzuku katika taasisi z elimu za afya ili kupata madaktari wakutosha na kupunguza tatizo la upungufu wa wauguzi katika zahanati mbalimbali.

Mbali ma serikali pia amewataka wananchi kuepukana na mzazamo finyu inayo sababisha kuamini kuwa vyuo vya Mbeya havina uwezo wa kufundisha kwa makini na kuachana na fikra hizo.

Aidha Mkwela alisema kuwa sasa elimu inategemeana na chuo kinavyo toa elimu na kujipanga katika utoaji wa elimu husika.

Alisema kumekuwa na utafauti mkubwa katika upande wa ghalama katika tasisi za serikali na za binafsi kutokana na utoaji wa ruzuku taasisi za kiserikali zina pata ruzuku kwa asilimia kazaa.

Alisema kuwa ili kupata madaktari wenye moyo wa kupenda fani hiyo kutokana na uhamasishaji kuanzia katika elimu ya msingi hadi sekondari kitu kitakacho saidia watu kuipenda taaluma hiyo ya udaktari na wenye wito.

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo cha St. John Health college, Bi. Adelhalde Haule alisema kuwa jamii inapashwa kutakua umuhimu wa kuwapeleka watoto wao katika taasisi za elimu ya afya ili kupunguza upungufu wa walaalamu hao wa afya.

 Alisema kuwa ili kupambana na changamoto za afya hapa nchini ni jambo la muhimu kujituma katika masomo ya sayansi na kuvitumia vyuo mbalimbali vya elimu ya afya vinavyo anzishwa jijini Mbeya.