WAZIRI ASHANGAZWA NA JENGO LA HOSPITALI





WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Hawa Ghasia, ameshangwazwa na ujenzi wa jengo la utawala wa hospitari ya wilaya ya Mbarali ambalo ni kubwa na kuwa la utawala bila ya sehemu za kutolea huduma kwa jamii za kiafya.

Mh. Ghasia akiwa katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya inayetekelezwa na serikali wilayanio Mbarali alishangwazwa na jengo hilo la utawala la Ghorofa moja ambalo linajengwa na serikali kwa ajili ya utawala wa hospitali ya wilaya ya Mbarali.

Akitolewa ufafanuzi wa ujenzi wa jingo hilo la utawala na mkandalasi wa wilaya ya Mbarali Vicent Komba ambaye alisema kuwa kulingana na ramani ya jingo hilo walivyo pewa inaonyesha kuwa jingo hilo litakuwa la utawala na kutakuwa na jingo lingine la hospitali.

Hivyo Mh. Ghasia alisema kuwa katika majengo ya utawala kuna kuwa na hospitali humo humo nah ii ni katika hospitali mbalimbali na jingo hilo nikubwa linaweza kufaa kwa kuwepo kwa huduma zingine.

Alitoa ushauri kwa mkandalasi wa wilaya kuligawa jengohilo kulingana na mahitaji ya hospitali na kuanzakutumika kama hospitali na utawala kama lilivyokusudiwa.

“Jengo hili ninaweza kutumika pia kama hospitali na utawala vitatumika vyumba vichache isipokuwa chumba cha kuhifadhia maiti na maabara haviwezi kuwekwa katika jingo la utawala,” alisema Ghasia.

Kwa upande wake mkandarasi wa wilaya, Vicent Komba alisema kuwa itawabidi kuzingatia ushauri huo na kuanza kuligawa jengo hilo kwamahitaji ya hospitali na kutenga vyumba vya ofisi za utawala.

Nae mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandolo alisema kuwa ni vima jengo hilo likikamilika litumika kama hospitali na wananchi wanajua jingo hilo ni hospitali na si utawala pekee.

Jengo hilo la utawala wa hospitali ya wilaya ya Mbarali lenye Ghorofa moja linatarajia kukamilika hivi karibuni na kuanza kutumika na kupunguza atha ya huduma ya afya.