SIASA NI MCHEZO UNAOCHEZWA NA WANAO UJUA KUUCHEZA



SIASA ni mchezo ambao unachezwa na watu wanao ufahamu huku watu wengi wanekuwa wakiucheza bila kujua mwanzo na mwisho wake na kujikuta wakiishia wasiko kujua.




Kwani kumekuwa na vyama vya siasa ambavyo vimeanzia Zanzibar na kaskazini ambapo vimekuwa na viongozi wa kitaifa kutoka huo viliko anzishwa.

Akizungumza na wakazi wa Nzovwe jiji la Mbeya meya wa halmashauri ya Ilala na diwani wa Ukonga kupitia CCM, Jery Silaa, alisema kuwa siasa inachezwa na watu wanaoifahamu katika historia ya hapa nchini hakuna chama kilicho anzia mkoani Mbeya.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakidanganywa na wanasiasa wanao tafuta ajila kupitia siasa na kuishia kuwachagua viongozi wasiao na viongozi katika dola.

Silaa aliwaambia wakazi wa Nzovwe kuwa wamekosea (wamebugi) kumchagua kiongozi kutoka katika chama pinzani wakati alikuwepo kiongozi wa wa chama tawala na kuwa walirubuniwa na wanasiasa.

“Wananzovwe katika uchaguzi wenu wa kumchagua diwani mlibuki kumchagua kiongozi wa chama pinzani kwani yeyehana sauti sana kama kiongozi wa chama tawala katika baraza la madiwani na ndiomana meya anatoka chama tawala kutokana na kuwa na madiwani wengi wa CCM” alisema Silaa
 
Alisema kutokana na kuwa wananchi wengi hawaufahamu mchezo wa kisiasa ndio maana badala ya kuchagua mbunge wa CCM wakachagua wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na viongozi wengi bungeni na rais anatoka CCM.

Alisema kuwekuwa na uvumi kuwa vyama vya pinzani kuwa CCM kuwa ni chama cha wazee mbona kuna madiwani wabunge wengi ni vijana hivyo wananchi waepukana na uvumi wa watu hao wanaowarubuni.

Zaidi ya wanachama 100 waliopewa kadi za chama hicho wakiwemo wananchuo mbalimali kutoka katika chuo cha MUST, TIA na na wakazi wa mkoa Nzovwe.