DIWANI ATOA SIKU SABA ZA KUITISHA MKUTANO WA MAPATO NA MATUMIZI




VIONGOZI wa kijiji cha Lupeta kata ya Swaya halmashauri ya wilaya ya Mbeya wamepewa siku saba na diwani wa kata hiyo waitishe mkutano wa wananchi ili wawasomee mapato na matumizi ya kijiji.
 
Diwani wa kata hiyo Julius Ntokani alitoa amri hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika kijiji cha Lupeta baada ya wananchi wa kijiji hicho kuto somewa mapato na matumizi kwa muda mrefu.

Wananchi hao hawajasomewa mapato na matumizi tangu mwaka 2009 na kuto jua nini kinaendelea katika fedha zao zilizoko katika kijiji.

Diwani   Ntokani aliwataka viongozi hao waitishe mkutano wa kusoma mapato na matumizi ndani ya siku saba ili wananchi wajue pesa zai ipo kiasigani na matumizi yake kwani ni mda mrefu sasa umepita.

Hata hivyo mbali na kutosoma mapato na matumizi kwa muda mrefu wananchi wamebaini kuwapo kwa kbadhilifu wa fedha za kijiji na kumtuhumi mwenyekiti wa kijiji hicho Ezekia Mwashiwawa.

Moja wawanakijiji wa Lupata Japhet Mwakosya, alisema kuwa ikifika siku ya mkutano viongozi hao watoe kitu kinacho eleweka na wasije wakaja kuwaletea maneno.

Imedaiwa kuwa moja ya mamo ambayo yamekuwa yakisababisha kutosomwa kwa mapato na matumizi ni kutokana na baadhi ya viongozi katika halmashauri ya kijiji hicho kijiudhuru.

Baadhi ya wananchi walihojo ni kwanini hauja itishwa mkutano wa kijiji na wakati kunabaadhi ya viongozi na wajumbe walikuwa wamejuhudhuru na kusababisha mtummoja kuwa na nyadhifa nyingi.

Hiyo alimtaka kiongozi huyo kujiudhuru (mwenyekiti) ili kupisha uongozi mpya ambao utachaguliwa upya na kijiji.

Diwani kujibu maswali hayo alisema kuwa wananchi wawe na subira hadi yatakapo somwa mapato na matumidhi ndipo watolewe katika uongozi kwani wakiwatoa mapema kamakuna ubadhilifu watashidwa kudai pesa zao.

Mwenyekiti wa kijiji hicho hakuruhusiwa kuzungumza chochote katika mkutano huo kwani yeye alikuwa ndio mtuhumiwa kwa tuhuma za kutosoma mapato na matumizi.