BODABODA WAFUNGA MWAKA KWA KUSAIDIA YATIMA



MADEREVA wa pikipiki maarufu Bodaboda wametakiwa kujiheshimu na kuheshimu kazi yao ili na jamii inayo tumia usafiri huo kuwaheshimu.
Hayo yamebainishwa katika funga mwaka ya madereva hao wa kanda ya Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya, na kamada wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani katika hafra fupi, alisema madereva hao wanatakiwa kijiheshimu wao wenyewe.

Alisema bodaboda wakijiheshimu wao na kuheshimu kazi yao hata jamii ambayo ndio wateja wao watawaheshimu kama usafiri mwingine.

“Kama dereva atavaa vizuri ataheshimu kazi yake na ofisi anayo fanyia kazi yake na akiwa na kauri nzuri kwa wateja ndio itakuwa kivutio kikubwa kwa wateja  na kujijengea heshima kila siku za kazi yake,”  alisema Athumani na kuongeza.

“Bodaboda ni kazi ambayo inafahamika kiserikali ambayo ili lenga zaidi katika kuwapatia vijana kazi na kukabilia na na tatizo la uhaba wa ajila unao likabili taifa,”

Alisema hakuna sababu ya eneo la bodaboda kuwa ni kijiwe cha matusi na watu watadhalau kwa kutokana na hali hiyo na kufanya jamii iwachukie.

Awali akisoma risara Mwenyekiti wa Bodaboda kanda ya Mbalizi, Filipo Mwasomola alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanachama ambao wanataka umoja wao uvunjike.

Mbali na hayo aliyema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakisema maneno mabaya na kumwaga sumu kwa wanachama wengine ili kuvuruga umoja wao na kusababisha ugumu katika utendaji wa kazi.

Hata hivyo hafra hiyo iliyo andaliwa na wanabodaboda hao iliambatana na kutoa misaada kwa watoto yatima kutoka katika mitaa mbalimbali ya mjimdogo wa Mbalizi.
Mnyekiti wa kanda hiyo Mwasomola alisema, zawadi hizo zimelenga kuonyesha upendo kwa watoto hao wanao ishi katika mazingira magumi na kutoa shukurani kwa mungu kwa kuwavusha sarana na kuwaepusha na ajali za barabarani.

Mwasomola aliongeza kuwa wwalitarajia kuwa na watoto wasio pungua 100 kwa bahati mbaya wamepata 76 kutokana na ukilitimba uliopo kwa baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa kwa kuwataka wapeleke barua zenye mihuri ili wawape watoto.

“Tulitarajia kuwa na watoto wasio pungua 100 lakini tumepata watoto 76 ambao watapatiwa sabuni ya kuogea na kufulia, mchele, na biskuti, ili kuuanza mwaka nao vizuri,” alisema Mwasomola.

Alisema kuwa vitu hivyo vinathamani ya zaidi ya shilingi laki ambapo ameona vivema wakafunga mwaka na watoto wanao ishi katika mazingira magumu na kuanzanao mwaka pia katika mwaka jana wamempoteza kijana mwenzao mmoja kwa ajali ya barabarani.