KITUO cha uwekezaji kanda ya nyanda za juu kusini kimebaini kuwapo kwa maporomokao yanayo weza kuzarisha umeme.
Akizungumza na Elimtaa hivi karibuni, Meneja wa kituo cha uwekezaji mkoa Kanda za nyanda za juu kusini, Daudi Riginda amesema kuwa kumegundulika maporomoko katika wilaya ya Ileje ambayo yanaweza kuzarisha umeme utaoweza kutumika katika wilaya hiyo.
Hivyo amewataka wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika maporomoko hayo ili kuwekeza na kuzarisha umeme ambao halmashauri ya wilaya ya Ileje ina weza kuingia ubia na muwekezaji huyo...
Riginda alisema kuwa halmashauri hiyo inaweza kukaingia ubia na muwekezaji atakayewekeza na hatimawe kuiingizia kipato halmashauri hiyo.
Mbali na kuingia ubia na wewekezaji pia umeme utakao zalishwa wanaweza kuliuzia shirika la umeme tanzania TANESCO na kusambaza kwa wananchi.
Pia Meneja Huyo ametoa wito kwa wawekezaji kuzitumia fulsa hizo za kuwekeza katika maporomoko na kuwasaidia wananchi kupata huduma ya umeme.
Alisema kuwa umeme unaoweza kuzalishwa katika maporomoko hayo unaweza kutosheleza katika maeneo ya wakazi wa eneo husika.
Aidha Riginda alisema kuwa pia mapiromoko hayo yanaweza kuwa katika moja ya vivutio vya utalii kwa wananchi ambapo yanaweza kuingiza pesa za kigeni kwa watanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)