IMEBAINIKA kuwa migogoro mingi kazini inasababishwa na waajili kutokuwa na mipango mizuri ya kazi ofisini.
Akizungumza na Elimtaa katika semina maalum kwa wafanyakazi na waajili iliyofanyika jijini Mbeya, Afisa elimu kazi na usuruhishi, Bw. Raban Magamba amesema kuwa taasisi hiyo ime kuwa imekuwa ikitoa elimu ya usuruhisi kwa waajili na waajiliwa.
Amesema kuwa kumekuwa na migogoro migi katika ofisi mbalimbali kutokana na waajili kutokuwa na mipango nizuri ama kuwa na mipango ila waajiliwa kutoitekeleza na kusababisha mgogoro.
Bw. Magamba amesema kuwa baadhi ya migogoro imekuwa ikitokana na kutotolewa kwa maslahi ambayo mfanyakazi alistahili kuyapata.
Aidha ametoa wito kwa waajili na wafanyakazi kufanya kazi kila mtu kwa nafasi yake ofisini ili kila mmoja aonekane yuko katika sehemu salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)