WAWEKEZAJI KUJENGA SHULE

WAWEKEZAJI wa mashamba ya kapunga wilayani Mbarali wanatarajia kujenga shule ya kisasa kwaajili ya kuwasomesha watoto wanao zunguka maeneo waliyo wekeza.

hayo yamebainishwa na Meneja wa kituo cha uwekezaji wa kanda ya nyanda za juu kusini, Bw. Daudi Riginda wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kuwa wawekezaji wa mashamba ya kapunga wanatarajia kujenga shule ya kisasa katika maeneo yao.

Amesema lengo la wawekezaji hao kujenga shule na kuimarisha uhusiano na wakazi wa vijiji vya jirani.

Wawekezaji wa kampuni ya kapunga wamekuwa na mgogoro na kijiji kinacho wazunguka na tatizo lao lina husu mipaka ya kampuni na wanakijiji.