ZAIDI ya watahiniwa 42,100 wa kidato cha nne Mkoani wameanza kufanya
mtihani wao jana huku Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Kaponda
akiwataka wasimamizi wa mitihani hiyo kuwa waadilifu ili kuepusha sifa
mbaya ya kufutiwa matokeo npamoja na walimu wenyewe kujishusha hadhi.
Kaponda amesema kuwa kati ya hao
watahiniwa 34,159 na wale wa kujitegemea ni 7,941 kwa mkoa
mzima wa Mbeya ambao tayari wameanza mitihani jana mapema.
Akizungumza na mwandishi wa ELIMTAA ofisini
kwake jana kuhusiana kuanza mtihani huo ,Kaponda amesema vituo vilivyopo vya
kufanyia mtihani ni 279 na idadi ya wasimamizi ikiwa 1,323 .
Amesema kuwa mtihani huo umeanza
vizuri katika maeneo yote hivyo niwaomba wasimamizi wa mitihani hii kuwa
waadilifu wazuri tunaomba kusiwepo na udangajifu wowote katika mitihani
hii ,hatutapenda tatizo hili lijirudie tena tunataka wanafunzi wetu wa Mkoa wa
Mbeya wasifanye kazi ya kufutiwa matokeo .
Akizungumza tabia ya kuvuja mtihani
Ofisa Elimu huyo alisema wamekugundua kuwa tatizo la kuvuja kwa mitihani
lipo kwa wasimamizi wenyewe ambao hushindwa kuwa makini wakati wa zoezi
hilo likiwa linaendelea la usimamizi wa katika vyumba vya mtihani.
Aidha Kaponda amesema kilichotokea
mwaka jana cha kufutiwa matokeo kwa baadhi ya shule za sekondari Mkoani hapa
kilidhalilisha sana serikali na walimu wenyewe hivyo ni muhimu walimu kulinda
heshima kwani tatizo hilo linatokea sehemu ndogo sana .
Mmoja wa wananchi wa kata ya Ilomba
.Atupele Musa amesema kuwa mtihani huo wa kidato cha nne umeanza vizuri hivyo
ni vema kusitokee udangajifu wowote wa mtihani kama inavyokuwa siku zote.
