KUCHELEWA kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa
hospitali ya Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kumesabishwa na uhaba wa
Kokoto katika Kampuni ya Congolo Mswisswi ambao ulisimama kwa muda
kutokana na Tazara kugoma hivi karibuni.
Imeelezwa kuwa hospitali hiyo
ilitarajiwa kukamilika mapema lakini tatizo kubwa likatokea upande wa Kokoto
ambazo ililazimika kuagiza Mkoani Kibaha ambako nako walikuwa wakitumia
grama kubwa.
Akizungumza na Rock Fm ofisini kwake
Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya ya Mbarali Eng.VenatThadei Komba kuhusiana
na ujenzi huo wa mradi wa hospitali kutokamilika mapema.
Eng. Komba amesema mradi huo kwa
awamu ya kwanza unategemea kukamilika mwezi Disemba mwaka huu na kwamba awamu
ya pili wameomba bajeti kwa kwaka huu na kwamba mpaka kukamilika kwake
wanategemea kutumia zaidi ya bi.1.5.
