Makamu wa rais wa Iraq Tariq Hashemi ameipinga hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi yake na mahakama ya Baghdad akisema hana hatia.
Hashemi akizungumza kutoka mjini Ankara Uturuki amemtuhumu waziri mkuu Nuri al Maliki kutoka madhehebu ya shia kuwa nyuma ya hukumu hiyo.
Kauli ya Hashemi imekuja baada ya mahakama ya mjini Baghdad kumuhukumu kifo baada ya kumkuta na hatia ya kuhusika na ugaidi katika kesi ambayo iliendeshwa mahakami humo bila ya mwenyewe kuwepo.
Al Hasemi ni mmoja kati ya maafisa wa ngazi ya juu wenye sauti katika madhehebu ya Wasunni na kuna hofu kwamba uamuzi huo wa Mahakama huebnda ukazusha mvutano wa kimadhebu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
