MZOZO WA SILI WAKALIWA KATIKA KIKAO CHA 21

Baraza linalohusika na masuala ya haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuzungumzia zaidi suala la mzozo wa Syria wakati wa kikao chake cha 21 kinachoanza leo kwenye makao makuu ya baraza hilo mjini Geneva nchini Uswisi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon pamoja na wanadiplomasia wengine wa ngazi ya juu wanalenga kuishinikiza zaidi serikali ya Syria kuacha umwagikaji wa damu dhidi ya raia wake.

Nchini Syria kwenyewe, watu kadhaa wameuwawa katika wilaya ya Alepo katika mashambulio ya vikosi vya serikali hapo jana.


Ndege za kivita za vikosi vya wanajeshi wa serikali zilishambulia eneo hilo baada ya waasi kuvamia makambi ya wanajeshi.