MAHABUSU WAGOMA KULA

MAHABUSU wa kituo  kikuu cha Polisi jijini Mbeya  leo asubuhi wamegoma kula chakula  wakidai kutotendewa haki ya kupelekwa mahakamani  tangu wiki iliyopita  kinyume na sheria  za haki za binadamu,mahakama  na Jeshi la Polisi kwa ujumla.

Mahabusu hao wamesikika wakipiga kelele za kudai haki ya kufikishwa mahakamani  huku wakidai wamechoshwa na vitendo vya baadhi ya askari polisi kudai rushwa ndipo waachiliwe hali inayosababisha kuendelea kuvunda katika mahabusu hiyo na hawaelewi hatma yao.

Baadhi ya ndugu na jamaa wa mahabusu ambao  wamefika kituoni hapo kwa ajili ya kuwapelekea chakula wakizungumza na Rock Fm kwa masharti ya kutotajwa majina yao wamesema kuwa ndugu zao wamegoma kunywa chain a wamekataa kupelekewa chakula hadi watakapohakikishia wanafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kuwekewa dhamana.



Kwa upande wake mkuu wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athuman amesema kuwa suala hilo hajafikishiwa na kuashidiwa kulifuatilia.