WANAWAKE mkoani Ruvuma wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya Tume ya Kukusanya Maoni ya Mabadiliko ya Katiba ili watoe maoni yao kuhusu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kundi la tano la tume hiyo, Profesa Mwesiga Baregu, kwenye mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika mjini Songea.
Profesa Baregu amesema kumekuwa na idadi isiyoridhisha ya wanawake wanaohudhuria katika mikutano ya tume kulinganisha na waliopo kwenye kata wanazofika, kwani takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu 8,915 waliojitokeza katika Wilaya ya Namtumbo na Tunduru wanawake walikuwa 1,949 tu sawa na asilimia 21.9 ya mahudhurio.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Walioba, amesema kuwa wananchi wengi wanaojitokeza kwenye mikutano yao wamekuwa wakilalamika kwamba hawaielewi katiba iliyopo, hivyo ni vigumu kuchangia, ingawa alisema wanaeleza mambo ya msingi yanayohusiana na katiba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
