Majeshi ya
waasi wa Syria pamoja na yale ya
serikali yanapambana kudhibiti eneo muhimu
linalodhibitiwa na serikali karibu na mpaka
na Uturuki.
Kamanda wa
jeshi la waasi Abu Saeed amesema kuwa waasi
wanapambana kudhibiti eneo la Wadi al-Daif katika
jimbo la Maaret al Nouman, ambako majeshi ya serikali
yameweka makombora ambayo yanafyatuliwa kuelekea
maeneo katika jimbo la Idlib.
Mapigano hayo
yamekuja siku moja baada ya kombora la
Syria kuanguka katika jimbo la Hatay
nchini Uturuki , na kusababisha Uturuki kulipiza
kisasi kwa kushambulia kwa makombora ndani
ya Syria.
Shirika la
kuangalia haki za binadamu nchini Syria
limesema idadi ya watu waliouwawa jana
Jumatatu nchini Syria imefikia 210 na
idadi hiyo imefikia watu 4,727 katika mwezi
wa Septemba
