TOKYO: IMF YATOA RIPORT MPYA YA HALI YA UCHUMI



KABLA  ya  mkutano  wa  kila  mwaka  wa  shirika  la  fedha la  kimataifa IMF  na  benki  kuu  ya  dunia, IMF imetoa ripoti  yake  mpya  kuhusu  hali  ya  uchumi  wa  dunia.

Inatabiri  kuwa  ukuaji  wa  uchumi  wa  dunia  utapungua katika mwaka  2013.

Ukuaji  wa  uchumi  wa  Ujerumani utabakia  katika  asilimia  0.9  na  unatarajiwa   kubakia katika  hali  yake  ya  kawaida  mwaka ujao.