SERIKALI
imeipongeza Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) kwa kuleta manufaa makubwa
kwa taifa kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa na migodi yake nchini
katika nyanja mbalimbali ikiwamo uchumi wa nchi na maendeleo ya jamii.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, baada ya
kufanya ziara ya mgodi huo uliopo Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Katika ziara hiyo, Masele pamoja na Naibu
Waziri wa Nchi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Charles Kitwanga, wametembelea
miradi mikubwa ya jamii ambayo inatekelezwa na mgodi huo kwenye sekta
mbalimbali ikiwemo elimu, maji na afya.
Masele
amesema mgodi wa North Mara kihistoria umekuwa na matatizo ya mahusiano na
jamii inayouzunguka, lakini hatua kubwa zimepigwa sasa kuboresha mahusiano na
vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
