MBEYA: KAJUNA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI UVCCM-MBEYA


UCHAGUZI wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya umemalizika na kupatikana vingozi wapya ambapo Aman Kajuna ameibuka kidedea baada ya kuwamwaga wagombea wezake wawili hivyo kufanikiwa kushika nafasi ya Mwenyekiti vijana.

 Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulikuwa ni vitisho kwa kila mgombea ulifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MIST) kilichopo mjini hapa.

Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema ambaye pia alikuwa ni Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo amesema nafasi ya Mwenyekiti  imechukuliwa na Bw.Kajuna amabye amepata kura 465 akifuatiwa na Bi.Mary Mwaijumba ameyepata kura 37 huku Bi.Lusekelo Malema akipata 35.

Amemtaja mshindi wa nafasi ya Baraza kuu la Vijana kwa kura 393, kuwa ni  Neema Mwandabila huku wapinzani wake ambao ni  Saul Mwaisenye amepata kura 184 na Richard Kayinga ameambulia kura 25.