NGARA YAGUNDUA CHANZO CHA HATI CHAFU

CHANZO cha Halmashauri ya Ngara kupata hati chafu kwa miaka miwili mfululizo imeelezwa kuwa imesababishwa na watumishi kufanya kazi kwa mazoea.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Constantine Kanyasu, amebainisha hayo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ( RCC) Mkoa wa Kagera wakati Mwenyekiti wa kikao hicho, Kanali mstaafu Fabian Massawe, ametaka kuelezwa sababu za halmashauri hiyo kupata hati chafu.

Kanyasu amesema wafanyakazi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kisingizio kuwa watumishi ni wachache, jambo ambalo halina ukweli.