Mkuu wa mkoa wa Mbeya BW.Abasi Kandoro amekaa na viongozi wa dini ya kikristo na ya kiislam kujadili kwa pamoja swala la migogoro ya kidini inayo jitokeza hapa nchini.
Kikao hicho kilicho fanyika katika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa ya Mbeya na kujadiliana kwa pamoja juu ya swala hilo na kusema kua anahitaji ushirikiano kutoka kwao ili waweze kutatua tatizo hilo kwani lina athiri kwa amani ya nchi.
Aidha mkuu wa Mkoa BW. Kandoro mbali na suala hilo la mgogolo wa kidini amegusia juu ya swala la ujumbe mfupi wa maandishi unaozungunzia mabomu ambao upo katika mitando ya kijamii kuwa ni uongo hivyo amewata wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya swala hilo.
Hata hivyo Rock Fm imeweza kuzungumza na mchungaji wa Christian Forum Amosi Igundu na amesema kuwa lengo la kikao hicho nikurinda amani ya watanzania na pia ametoa wito kwa wananchi na waumini wa dini zote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)