MBEYA: MAENDELEA YANAKWAMA KWA KUTO TUSHIRIKISHA

KUSUASUA kwa shughuri za kimaendeleo katika kata ya Iganzo iliyopo Halmashauri ya jiji la Mbeya imedaiwa kunasababishwa na kukosekana kwa ushilikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya kimaendeleo.


Wakizungumza na rock fm kwa nyakati tofauti wananchi wa kata hiyo wamese kuwa wamekuwa wakishindwa kushilikishwa katika maamuzi ya shughuli za kimaendeleo hali inayo sababishwa na baahi ya wajumbe wamitaa kushindwa kuitisha vikao vya kujadili upitishaji wa maamuzi yatakayo epusha migogoro katika utekelezaji.


Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bw Oswege Furika amesema swala hilo lipo ndani ya kata yake na kwamba linatokana na wajumbe wa mitaa katika kata hiyo kutotoa  fulsa kwa wananchi hao kushiliki katika kutoa na kupanga njia bora za kufikia hitima mbalimbali za kimaendeleo.


Pamoja na hayo Diwani Fulika amesema yeye kama kiongozi wa kata hiyo anao wajibu wa kuhakikisha kila mwananchi wa kata hiyo anashilikishwa kikamilifu katika kupanga na kuratibu shughuri zote zinazo husu  maendeleo.