MPANGO wa taifa wa damu salama kanda ya nyanda za juu kusini umekuwa uki kabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuzwa kwa damu ambayo hutolewa bure.
Akizungumza na ELIMTAA mkuu wa kitengo cha damu salama Nyanda za juu kusini Dakta Savia Kundael amesema kuwa changamoto ambazo wanakutana nazo katika kutoa huduma hiyo ni malalamiko ya kuuzwa kwa damu, mila potofu, dini ambazo hazikubali kuongezwa damu,na watu kuwa na uelewa mdogo kuhusu huduma hiyo ya damu salama.
Amezitaja sifa za watu ambao wanaweza kuchangia damu ni mtu yeyote mwenye akili timamu, ambaye ametimiza umri wa miaka 18, na afya njema, wala magonjwa ya kurithi, na ambaye hatumii dozi ya muda mrefu.
Aidha Dakta Kundael amesema kuwa wanawake wanaweza kuchangia damu kila baada ya miezi minne na wanaume wanaweza kuchangia damu kila baada ya miezi 3 baada ya kutoa damu kwa mara ya kwanza.
Hivyo dakta ametoa wito kwa watu wote wenye sifa ya kuchangia damu kuweza kuchangia ili waweze kuokoa maisha ya watu wengine ,na pia amesema kuwa kwa wote wenye tabia ya kuuza damu au kutoa rushwa ya damu waache mara moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)