MALIASILI YAPATA MKURUGENZI MPYA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, amemteua Profesa Alexander Songorwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Idara ya Wanyamapori, akichukua nafasi ya Obeid Mbangwa, aliyetimuliwa kazi na Khamis Kagasheki.

Msaidizi wa Mbangwa ni Bonaventura Midala na watendaji wengine ambao wamesimamishwa kazi baada ya kubainika kuhusika katika kashfa ya utoroshaji wanyamapori hai kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda nje.

Taarifa ya Katibu Mkuu kwa vyombo vya habari, imetolewa na msemaji mkuu wa wizara hiyo, George Matiko, imeeleza kuwa kabla ya utezi huo, Prof. Songorwa amekuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) cha Morogoro na amekuwa Mkuu wa Idara hiyo ya usimamizi wa Wanyamapori chuoni hapo.

Tarishi pia amemteua Profesa Jafari Kideghesho kuwa Mkurugenzi Msaidizi, kuiongoza sehemu ya matumizi endelevu ya wanyamapori.